-->

Exclusive: Maskini Jini Kabula! Ukimsikia Utalia, Anatia Huruma (Video)

Ikiwa ni takriban miezi miwili na siku kadhaa tangu kuzagaa kwa ishu za kuugua ugonjwa wa afya ya akili ukiambatana na kuchanganyikiwa kwa mwigizaji wa sinema za Kibongo, hasa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, hatimaye ameibuka na kunena mambo mazito yenye kuumiza juu ya sakata hilo.

Miongoni mwa mambo anayodai kutendewa, Kabula alisema kuwa, alilazimishwa kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi ‘ngoma’ kisha akaanzishiwa dozi ambayo hakuwa anajua kinachoendelea.

MACHOZI KABLA YA SIMULIZI

Muda wote Kabula alikuwa akitiririkwa na machozi yaliyobeba hisia na kila tafsiri ya uchungu huku akitamka maneno mengi makali kwa mfululizo (busara imetumika kutoyaanika).

MKASA WENYE KUUMIZA

“Ninakumbuka siku hiyo nilitoka kanisani, wakati huo nikiishi kwa dada aitwaye Angel. Nilipofi ka nyumbani nilishangaa kukuta watu wengi, nikashtuka kwa kudhani kuna msiba, lakini ghafl a nilikamatwa kwa nguvu na kufungwa kamba.

“Niliuliza kuna nini, lakini hakuna aliyenijibu, zaidi ya baadhi yao kuanza kulia. “Nilikuwa na nguvu sana, maana ndugu zangu wa Marekani akiwemo pacha wangu, Mwanamuziki Rihanna wa Marekani (hapa stori inaanza kuwa mchelemchele) walikuwa wameshatuma makombora kuja kuniokoa mimi malaika niliyezaliwa Tanzania kwa bahati mbaya ili kuja kuikomboa nchi hii.

“Wakanipakiza kwenye lori na kunipeleka Muhimbili (hospitalini). Nilikuwa ninalia sana huku

nikipambana nao kwa nguvu zote, kiukweli nilichoka sana jamani (machozi). “Nimeteswa na kuumizwa sana, eti mimi ninaitwa kichaa, kweli eti (jina la mwandishi), mimi ninaweza kuwa

kichaa kwa unavyonifahamu supastaa mkubwa Bongo? Aah! Hii dunia ni katili sana, lakini Mungu hashindwi na jambo,” ndivyo alivyoanza kusimulia Kabula na kuendelea:

SIMULIZI INAKOLEA SASA

“Wakanipeleka Muhimbili. Lakini kabla ya hapo walishanichoma sindano yenye dawa kali na kunilegeza mwili huku wakinilazimisha kumeza dawa, Mungu anajua (kilio).

“Hapo nikapitiwa na usingizi. Nilipozinduka nilijikuta hospitalini, lakini sasa Wamarekani walikuwa wamekizunguka kitanda changu huku wakirekodi matukio yote (picha limeanza mchelemchele tena). “Basi wakaniuliza kama ninalifahamu eneo hilo, nikawajibu ni Ocean Road (Hospitali ya Saratani), wakaitikia ni kweli japokuwa baadaye nilikuja kujua kwamba ni Muhimbili, yaani walinifanya kama zuzu au mdoli mdogo.”

AFUNGIWA WODI YA VICHAA

Kabula aliendelea kusimulia; “Eti cha ajabu nikafungiwa kwenye wodi ya vichaa. Huko nilikutana na giza la ajabu (kimya, kilio na kigugumizi cha hasira). Kulikuwa na wachawi wakiwa uchi wa mnyama, wakijisaidia karibu kabisa na nilipoweka uso wangu. “Ilikuwa kama nipo kuzimu, lakini hata hivyo, nilijitambua kuwa mimi si Mtanzania ila ni Raia wa Marekani na hata Rihanna ambaye ni pacha wangu nilishamwambia, akasema atakuja kurusha makombora ya ajabu nchi nzima iteketee (mchelemchele tena).  “Nikafungwa kwa minyororo, hebu ona nilivyoumia jamani (akifunua gauni na kuonesha alama za kufungwa eneo la mapajani na makovu sehemu mbalimbali mwilini).

ALIFANYIWA HAYA PIA

“Eti nilipimwa damu na kuambiwa nina Virusi Vya Ukimwi, nikapewa vidonge vya kumeza na mimi sikuwa na jinsi zaidi ya kupokea ili niwafurahishe lakini ukweli sina Ukimwi. Kwa kweli sijawahi kupitia kwenye kipindi kigumu kama hiki, wananionea wivu tu kwa kuwa mimi ni mzuri na mrembo kuliko mama yao yule ambaye walimvisha matambara meusi mbele ya moto mkubwa (mchelemchele tena).

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364