-->

Mzazi Mwenzake Linah Afungukia Picha Tata

Baba mtoto wa msanii Linah Sanga, Mchomvu amedai picha alizopiga msanii huyo akiwa mjamzito ni za kawaida na kwamba alihusika kwa asilimia zote kuhakikisha zoezi linaenda sawa ikiwa ni pamoja na kuandaa mavazi, ingawa kwa jamii ilionekana tofauti.

Aidha ameongeza kuwa picha kama zile kwa Linah ambaye ni mwanamuziki hazina shida hata kidogo ingawa kwa jamii ya kiafrika zilionekana hazina maadili na kuongeza kwamba watanzania wanapenda kuviona vitu hivyo kwa wasanii kutoka nchi za magharibi tu na vikifanyika hapa ndani inakuwa ni uvunjaji wa maadili.
“Mimi kwangu picha zile nilizichukulia kawaida sana kutokana na kazi yake anayoifanya Linah. Linah ni msanii lakini pia alikuwa na furaha ya kupata mtoto. Mtu wa kawaida akipiga zile picha nitamshangaa hata mimi. Lakini picha hizi hizi wanapiga kina Beyonce, na mashabiki wanataka wasanii wetu wafikie levo zile kwa hiyo watulie ndipo tunapoelekea. Lakini niweke wazi mimi nilihusika asilimia zote ikiwa ni pamoja na yale mafuta ambayo watu walikuwa wanajiuliza nani kampaka. Linah hakuwa anataka mtu mwingine auguse mwili wake ndiyo maana nilikuwa naye karibu kila wakati,” alisema


Akizungumzia kuhusu ushirikina kutajwa kama chanzo cha Linah kuchelewa kujifungua, Mchomvu amefunguka na kusema hakuna ushirikina uliohusika kuchelewesha mama mtoto wake kujifungua kwa sababu ya kupiga picha zilizokuwa zikimuonesha sehemu kubwa ya tumbo lake wazi na kutaka watu waelewe ni mambo ya kawaida yanayotokea kwa mama mjamzito.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364