-->

Faiza Ally Afungukia Kiki za Bongo Movi

Msanii wa filamu Faiza Ally amewataka wasanii wenzake wa filamu kuacha kutafuta ‘kiki’ ambazo haziwanufaishi katika kazi zao.

FAIZA ALLY78
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Faiza amesema wasanii wengi wa kike wa filamu wanatafuta kiki za mapenzi bila kujua kiki hizo zitawasaidiaje.

“Kiki sio mbaya lakini hiyo kiki inakusaidiaje?, mimi ukiona nafanya kiki ujue kuna kazi ambayo inakuja, sio kufanya kiki alafu unakaa kimya ilimradi uonekana na wewe upo, kwa hiyo mimi ningewashauri wasanii wenzangu wa filamu tufanye kazi,” alisema Faiza.

Muigizaji huyo kwa sasa anajipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Baby Mama Drama’.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364