-->

Faiza Ally Afungukia Mavazi Yake na Kushauri Mambo Haya Matatu!

Faiza Ally

Inawezekana kuvaa nguo fupi au bikini ni tatizo hasa ktk upande wa imani zetu kutokana na maamrisho ya vitabu.
Lkn Lkn hakuna tatizo kubwa kuliko kumtangazia mtu sifa mbaya – unapo sema maneno mabaya unatengeneza sumu mbaya sana kwenye mioyo na fikra za watu…tofauti na yale mavazi maana akisha vaa anavua mwisho wa siku ni mavazi tu ambayo hayamzuru mtu yoyote kwa namna yoyote lkn maneno mabaya na sifa mbaya yana haribu fikra za watu na mioyo ya watu nakupelekea kuharibu watu na kudumu kwenye vizazi na vizazi.
Jamani tuchungane kila mtu awe balozi wa mwenzie kumuongelea mazuri – kwa nini watu wanatangaza sana habari mbaya ikiwa na nzuri wana zifahamu ? inamaana katika huyo mmbaya unae mtangazia mabaya hata zuri moja hana? Binaadamu tusiwe wepesi wakusikiliza ya watu naku yachukulia kweli na uhakika na kuendeleza.
Ninacho shukuru M.Mungu Kila anae pataga nafasi ya kunijua huwa anatoka na faida na kuweka tofauti ya kile alicho sikia juu yangu – kitu ambacho huwa kinanipa nguvu ya kuendelea kuwa mimi bila kujali binaabu wanataka nini……… ! Baada kusema haya na kushauri mambo matatu.
1 : Kuwa wewe na simamia kile unacho kiamini
2: Kuwa mkweli na uwe mwenye kupenda haki na usawa.
3: Jiamini ……jikubali …. Jiongeza…jikaze ….jidhamini na ujikubali
#USITETERESHWE NA WALIMWENGU INAWEZAKANA KABISA NI UJINGA WAO BILA KUJALI UMRI WAO MAANA KUNA WATU WAZIMA PIA WAJINGA NA HUKO NDIO SUMU ZILIPO TOKEA ZIKAENEA KWENYE VIZAZI VIPYA- HIVYO SI KILA MTU MZIMA NI MUELEVU ?

Faiza Ally @faizaally_on instagram

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364