Faiza Atumia Njia Hii Kumfikishia Ujumbe Baba wa Mtoto Wake ‘Sugu’
Staa wa Bongo Movies, Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenzie na Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameamua kutumia mtandao wa instagram kumfikishia ujumbe mzazi mwezie kuhusu matunzo ya mtoto kwa madai kuwa kwa sasa hawana mawasiliano.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo, Faiza aliweka video ya mtoto wao Sasha akimuomba hela baba yake (Sugu) yakusukia nyewele na kisha Faiza akaandika;
“Anae mjua baba wa huyu mtoto amwambie analilia kusuka….. Anaomba baba yake amtumie hela kwa kuwa sina mawasiliano nae hopeful mtamfikishia ujumbe….. Na mimi ndio hivyo tena leo sina chapaa”
Kitendo ambacho mashabiki wengihawakukiona kama ni cha kiungwana;
- prak_wa_mbuluDuh umejidharirisha sana We mdada wanawake wenzio tumezalishwa na wanaume hawajulikan walipo na tunawalea watoto wetu bila matangazo kwa public kwann we,halafu ni hela ndogo sana tena ya kusukia dah.ingekuwa Ada je? Badilika Dada, wanawake tunaweza sana
- mimadully@suzanrichard26 mm cku zooote namuunga mkono huyu mwanamke mwenzangu kwa mapitio yake lkn ingekuwa vema kama mtt angekuwa na shida ya ada lkn anataka.pesa ya kusukaa .kwan sh ngap najua hela unayo ila tuu umetaka kufanya hivi .mamii wataala wanasema ukiwa unamzungumzia ulieachana nae ina maana bado unampenda.@faizaally_ hata mm nalea mtt wangu mwenyewe na combi hata sent.kwa baba yake.acha mamiiii potezeaaaaaa
- nancychessyDaaaahh hata kama faizaaa wazazi tujifunze kutowaonyesha watoto udhaifu wetu kusuka ni kitu kidogo msifikie huko nyie ni wazazi moto mnaouchochea anaeumia ni mtoto hapo unapandikiza sumu Dada u re 32 umepitia mangapi?! tembo hashindwi na mkonga wake
- bahati_festoDuuh sugu kwanini unafanya hivyo hiyo ni damu yko jalibu kufikilia mara mbili
- ashanour15Jamani sugu alishazungumza bungeni namna anavyomhudumia mwanae sasha kuanzia ada ya shule na mengine,faiza acha utoto unaona kama unamdhalilisha sugu lkn its shame to u,hakuna atakae kubaliana na wewe kwamba sugu amekosa hela ya kumpa mtoto akasuke,!!!
- mona_longwayeye openin,sidhan km huy dada ana shida na hela ila hii ujumbe kw jamii anajarib kuwaonyesh watu ukwel kuhus jinsi wanawake wanavyokosa msaada upande wa pili
- davidmwaikamboHivi kweli mwanao unaweza kumuweka instragram kisa kusuka nywele
Baada ya watu wengi kuonekana kupinga kitendo hicho, Faiza aliibuka tena na kuandika;
Nyinyi mnaosema kama nimeshindwa kumlea mtoto nimuachia baba yake- nawaona wapumbavu tu kama wapumbavu wengine wote….. kutaka kuishi na mwanangu sio sababu ya baba kutokujua mtoto ana kaa wapi! anakula nini- ada anapata wapi na shule ana soma wapi…ndio nina haki ya kukaa na mwanangu lkn sio kwamba kwa sababu naishi nae ndio sababu ya kutomkutunza mwanae…. na pumbavu zenu wale wanao sema na mzalilisha sasa mntaka nimpeje ujumbe ikiwa sina mawasiliano nae ? kama sio kutumia mitandao ….. ? nao mnaosema nimeshindwa mnajua nalipa kodi kiasi gani? ada sh ngapi ? matumizi na mnajua napataje manina zenu? au mnazani kuwa single mama mchezo – pumbavu zenu nyote mnao shangaa mimi kuonyesha hisia zangu….. kuna nyakati zingine unashindwa kujizuia ukiwa kama mzazi unapo kosa msaada wowote kwa mzazi mwenzio special akiwa na uwezo wa kutoa…. na si kwamba nimeshindwa ila nimekasirika na kusikitika sana pale mwanangu anapo hitaji na nakua sina kwa wakati huo na nikitizama baba yake anao uwezo lkn ana nikomoa kwa ajilia ya kumuacha – hii haingiliani kabisa na kuto kumjali mwanao- na zaidi akiwa amesimama bungeni kutetea wananchi ikiwa vizazi vyake vina hangaika ikiwa kaka yake sasha ambae amemtoa mjini baada kujulikana na kumpeleka mtwara amekua mlevi huko wkt bora angemuacha hapa garage alikua ana jipatia riziki yake …… wanae wote wawili hawajali ….. kama mzazi inauma …… nyio msio jua uchungu wa mtoto wala ugumu wa kuwa singo maza fungeni midomo yenu visebengo wakubwa subiri yenu !!!!!!!!!!! na baada ya yote kunipeleka mahakani natoa hela zangu na kesi inazungushwa….. kila ninapo fika mahakamani lzm nilipe na ada ya mwanasheria m.2 …… kama sio kukosa ubinaadamu ni nini ????? – sikilizeni sina asili ya kitumwa niko katika taifa huru na nitasema na kufanya kile ninacho amini….. na nina amini kiongozi bora ana anzia nyumbani……….. lkn mwisho wa siku yote maisha nitasimama tu na nitaweza lkn wkt mwingine binaadamu lzm tuseme yaliyo moyoni ili tuendelee na yajayo…… narudia tena kwa yoyote anae shangaa hili ni mpumbavu na ametoka kwenye familia za kinafki zinazo funikaga vitu ambavyo havi stahili kufunikwa!!!!!!!!!!!!!
Neno moja kwake.