Prezzo Akanusha Kutaka Kumuua Mke Wake
NYOTA wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘CMB Prezzo’, amekanusha taarifa kwamba anamtishia kifo aliyekuwa mke wake, Michelle Yola.
Wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya kulikuwa na taarifa kwamba Michelle anatishiwa kifo na mkali wa mavazi ‘King of Bling’ Prezzo, lakini msanii huyo amekanusha na kusema Michelle anatafuta kiki.
“Niliweka wazi kuwa sina muda wa kumfuatilia mtu, nipo napambana na hali yangu kwa ajili ya maisha ya baadaye, hivyo nashangaa kuona habari kuwa ninamtishia kifo Michelle.
“Kila mmoja ana mambo yake, hivyo sina muda huo, inawezekana akawa anatafuta kiki kupitia jina langu, mimi na yeye mipango yetu ya kuwa pamoja ilikwisha, hivyo sitaki kusikia mambo kati yangu na yeye,” alisema Prezzo.
Mtanzania