Filamu ya ‘7314Munu Mukuru’ Kutoka Mwezi Huu
BAADA ya kufanya vizuri kwa filamu ya ‘Mr. Makuka’ msanii wa filamu Tanzania, Bakari Makuka ‘Beka’, yupo mbioni kuachia filamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘7314Munu Mukuru’.
Beka alisema katika filamu hiyo amewashirikisha wasanii wakongwe akiwemo, Fatuma Makongoro, ‘Bi Mwenda’, Chuchu Hans, Haji Salum ‘Mboto’, Pacho Mwamba na wasanii wengine wengi.
“Filamu hii nataraji kuiachia mwishoni mwa mwezi huu, nimetumia mazingira halisi kulingana na hadithi inavyotaka hivyo ni vyema Watanzania mkapata filamu za uhalisia badala ya zile zinazoigwa kutoka filamu za nje,’’ alisema Beka.
Beka mpaka sasa ameshatoa filamu tatu, mwaka 2014 alitamba na ‘My Boss’, mwaka 2015 alitoka na ‘Mr. Makuka’ na mwaka huu anataraji kutoka na filamu ya ‘7314Munu Mukuru’ inayobeba jina la kilugha.
Mtanzania