-->

Lady Jaydee Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake

Msanii wa siku nyingi wa Bongo Fleva hapa nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee amewaomba watanzania wampende yeye kama yeye na si kumfuatilia kuhusu mahusiano yake kimapenzi.

Lady-Jaydee-life_0

Jaydee ameyasema hayo katika kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa baada ya mtangazaji Sam Misago kumuuliza swali kwamba kuna tetesi kwamba karudiana na mpenzi wake wa zamani Gadner.

”Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania wanipende kama mimi kama Jaydee na si vinginevyo”-amesema Jaydee.

Msanii huyo ameibuka upya na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndi ndi ndi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364