Filamu ya Baba na Mwana ni Kali Sana – Kinye Mkali
KINYE Mkali mkurugenzi wa Kinye Mkali Picters amejisifia kuwa filamu yake ya Baba na Mwana ni sinema ya kipekee na haina mfano wake kwani ni kazi ambayo ameifanya kwa umakini mkubwa na itasambazwa na kampuni hiyo nchi nzima.
“Kila siku tunajitahidi kufanya kitu kilicho bora zaidi hasa katika masuala ya burudani na elimu kwa jamii, ndio maana unakuta filamu ninazotengeneza mimi zinafurahisha na kuelimisha hilo unapata katika filamu ya Baba na Mwana.’anajisifu Kinye.
Sinema ya Baba na Mwana ni kazi yenye hadithi ya kusisimua na ina wasanii nyota na wenye vipaji kutoka Kinye Mkali Pictures mabingwa wa Komedi Bongo wanaotengeneza filamu na kusambaza jijini Dar es Salaam.
Filamu ya Baba na Mwana inatoka leo jumatatu ya tarehe 4th April 2016 na kusambazwa nchi nzima katika maduka yote yanayouza sinema za kibongo si ya kuikosa kabisa kuwa wa kwanza kununua filamu ya kitanzania nakala halisi na si Dvd fake.
FC