Nuh Mizwanda Atoboa Alichokuwa Akikifanya kwa Shilole
Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Shilole, Nuh Mziwanda amedai wakati yupo kwa Shilole alikuwa hafanyi muziki bali alikuwa akifanya mapenzi.
Akizungumza katika kipindi cha Clouds E, Jamatatu hii, Nuh alisema hali hiyo ilimfanya apotee kimuziki na kukiki zaidi kimapenzi.
“Kwa Shilole nilikuwa nikifanya mapenzi sio muziki, ndio maana ukaona kwenye upande wa muziki sikuwa vizuri,” alisema Nuh. “Hata followers wetu walikuwa wanakuja kuangalia mapenzi na sio kwa ajili ya muziki. Ndio maana alikuwa anashindwa hata kunishauri kuhusu muziki wangu, kwa sababu kama angekuwa ni mtu sahihi angekuwa ananishauri kwenye masuala ya kujenga,” alifafanua Nuh.
Nuh amesema kwa sasa amejipanga yeye kama yeye kuachia kazi yake mpya ya kuimba pamoja na ya kurap.