Filamu ya Kisogo ya Gabo na Wema Sepetu Kuruka Dunia Nzima
FILAMU ya Kisogo ya mwuigizaji nyota Bongo imekamilika na inatarajia kuonekana Dunia kote kwa njia ya kisasa kabisa akiongea na FC Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ anasema kuwa sinema ya Kisogo imetengenezwa katika teknolojia ya kimataifa na hivyo itaweza kubadilisha soko la filamu Bongo na kuweza kufika katika anga za kimataifa kwani ni kazi yenye mvuto na hadithi ya kusisimua huku akijivuani washiriki wa sinema hiyo ya Kisogo.
“Nilikuwa kimya hakuna mtu aliyejua Gabo anakuja na kitu gani katika filamu, nilitrumia muda mwingi kufanya utafiti na kugundua kuwa wateja wanahitaji kupata kitu ambacho kinaburudisha, kinaelimisha lakini bila mtu kufika Kariakoo aua katika maduka ya kuuzia filamu, sasa tunakuja Mobile App Uhondo,”alisema Gabo.
Gabo anasema kuwa mfumo ambao unatamwezesha mteja kupata filamu za Gabo ni Kisogo na kazi nyingine ambazo anatarajia kuzimalizia katika kurekodi hivi sasa, katika filamu ya Kisogo wasanii nyota pamoja na watu mashahuri wameshiriki ni pamoja na Millard Ayo, Wema Sepetu, Gabo Zigamba mwenyewe, H. Baba na wasanii wengine wanaotamba na filamu kubwa Bongo, Filamu ya Kisogo inatarajia kuzinduliwa hivi karibuni.
Kisogo ni filamu fupi ambayo ina kisa cha aina ya kipekee na inagusa jamii yetu moja kwa moja na mtayarishaji wa sinema hiyo Gabo anasema kuwa walifanya hivyo kwa ajili ya kuweza kufikisha ujumbe na elimu kwa watazamaji ambao asilimia kubwa ni wamiliki wa simu za mkononi hivyo mtu yoyote ana haki ya kuona filamu hiyo kupitia simu yake.
Filamu Central