Gabo Ajifananisha na Trump
Muingizaji wa Bongo Movie Gabo ambaye alishinda tuzo mbili usiku wa EATV AWARD ikiwemo tuzo ya muingizaji bora wa kiume na filamu bora ya mwaka amesema anajiona kama Donald Trump baada ya kushinda tuzo hizo.
Akipiga story ndani ya eNewz, Gabo amesema anaamini kwa sasa ni wakati wake na matumizi sahihi ya akili ndo yanaweza kukupeleka popote unapotaka kufika na anasema ufanisi wa filamu yake na ilivyoweza kufikishwa kwa watu ndo iliongeza ubora wa filamu yake.
Hata hivyo Gabo amesema soko la filamu haliko rasmi ila kama likiwa rasmi kuna watu wanaweza wakafanya vizuri zaidi ya sasa kwa kuwa kuna watu wakiwezeshwa wanaweza na anatarajia kupata tuzo nyingi zaidi kila mwaka.