-->

Gabo Awafunda Wanawake

Muigizaji anayefanya vizuri sana kwenye ‘game’ ya bongo movie ametoa somo kwa wanawake wa kiislamu kuacha kubweteka na kuwa wachafu kwa kisingizio cha mwezi wa ramadhani kwani watawapatia mianya wandani wao kuchepuka.

Gabo amefunguka hayo kwa kudai kuwa wanawake kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan wamekuwa wakijiachia kwa kusingizia kuwa wanafanya maandalizi ya futari na kujishughulisha muda mwingi jikoni.

“Utakuta mwanamke toka saa 6 anapika futari mpaka Magharib adhana yamkuta jikoni nywele kitimutimu dira limejaa unga wa ngano umegandia na nyanya anamtengea mume chakula ananuka kachori na katlesi,unapika futar nyingi mpaka ukilala hoi. Kuna wanawake Ramadhan basi wanajiachiaga wanakuwa rafu ukiuliza kafunga, shauri yenu hakuna kipindi wanaume wachepuka kama mwezi huu” – Gabo Zigamba.

Gabo ameongeza kwamba “Kufunga sio sababu ukawe rafu pika futar kiasi upate muda wa kufanya ibada zako na kuhudumia ndoa yako, pika kiasi wee siku moja futar 10 bado uji chai juice pika mapema koga chana nywele zako kama mwehu badilisha hilo dira lako lilogandia unga wa ngano”– Gabo alipigilia mstari.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364