-->

Gabo Zigamba Aishauri Haya Serikali

Msanii Salim Ahmed alimaarufu kama ‘Gabo Zigamba’ ameishauri serikali ya awamu ya tano kutolea macho kwenye sekta ya kilimo Tanzania pamoja na vipaji na kusema kuwa hivyo ndivyo vyanzo vizuri vya mapato.

gabo89

Gabo Zigamba

Gabo Zigamba ametumia ukurasa wake wa Instgram kutoa ujumbe huo kwa serikali na kuiomba serikali ya awamu ya tano iweze kutilia mkazo katika mambo hayo kwani yamekuwa ndiyo chanzo kizuri cha mapoto.

“Mkulima na mtu mwenye kipaji ndiyo chanzo cha mapato ‘Please my Government’ tupieni macho hapo.” alisisitiza Gabo Zigamba

Mbali na hilo Gabo Zigamba amedai kuwa malengo pekee hayaweze kusafisha njia na kufikia mafanikio ya kila jambo unalotaka kulifanya bali ni juhudi binafsi za mtu ndizo zinaweza kumfikisha mtu sehemu, kwa kutolea mfano yeye mwenyewe.

“Lengo halisafishi njia ila juhudi zangu binafsi na msaada wa Mungu wangu umenifkisha mimi hapa nilipo leo lakini hakuna anaejali, bali wapo watu wanao ifaid thamani yangu” alisema Gabo.

 eatv,tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364