-->

Gabo Zigamba:Matapeli Wanatumia Jina langu

Wezi wa mtandaoni wameonekana kutembea karibu na msanii nguli wa Bongo movies, Gabo Zigamba ikiwa ni siku chache tangu walipoidukua akaunti yake ya facebook.

gambo02

Msanii huyo ametoa tahadhari kuhusu utapeli unaoendelea kwa kutumia jina lake.

Awali, msanii huyo alipoteza simu mbili za mkononi ambazo baadaye zilionekana kutumiwa na matapeli hao kuomba misaada kwa watu mbalimbali wakijifanya kuwa wao ndio Gabo.

Kadhalika, juzi akaunti ya Facebook ya msanii huyo ilidukuliwa na kutumiwa kwa muda na matapeli hao kwa kujifanya ndio msanii huyo. Hata hivyo, hatimaye alifanikiwa kuirejesha akaunti hiyo katika himaya yake.

“Nahisi mimi ndio msanii ninayeongoza kwa jina langu kutumiwa na matapeli kwa sababu nimekuwa nikipata taarifa mbalimbali kuhusu watu wanaolitumia,” amesema Gabo na kuongeza:

“Kwa mfano kuna binti mmoja aliyejifanya ndiye Gabo na amekuwa akitapeli kwa kudai anauza mabegi”.

Msanii huyo ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia majina ya watu wengine, hususan wale maarufu kwa minajili ya kutapeli.

Amesema kuwa yuko kwenye mchakato wa kufungua akaunti zake mpya za mitandao ya kijamii.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364