-->

Jengua Afunguka Haya Kuhusu Kukuza Vipaji vya Wasanii Wachanga

Mzee Mohammed Fungafunga maarufu katika tasnia ya filamu kama Jengua amefunguka na kusema anaweza kufanya filamu hata bure ili kuwasaidia wasanii wachanga waweze kutoka katika tasnia ya filamu nchini.

jengua

Amesema anafanya hivyo kwa kuwa anatambua kuwa ni lazima waweze kukuza watu wengine kwenye tasnia ya filamu kwani wao umri umeshakwenda.

Mzee Jengua alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz cha EATV na kudai kuwa ameshawahi kufanya kazi bure kwa lengo la kuwasaidia wasanii wachanga ili waweze kutoka kwenye filamu.

“Nimekuwa nikitokea kwenye filamu nyingi sana kwa sababu mimi nimekuwa nikishirikiana sana na hawa wasanii ‘Underground’ japo mimi sisemi katika nchi hii kama kuna ‘Underground’ wote tuko sawa sema sisi tumepata bahati tu ya kuweza kuonekana, hivyo mimi nashirikiana sana na hawa wasanii wachanga ili kuweza kuwakuza wao, kwani nikikumbuka hata mimi nimekuzwa na wasanii wakongwe enzi hizo kama Mzee Kipara, Mzee Rajabu Hatia, Pwagu yaani walitupatia material yao bila tatizo hivyo na mimi naona napaswa kufanya hivyo, mimi kuna filamu nacheza hata bure ili kuwasaidia hawa wasanii wachanga na wao waweze kutoka” alisema Mzee Jengua

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364