Nisha Awatolea Povu Kina Marioo
Muigizaji wa filamu bongo na Mchekeshaji, Nisha amewatolea uvivu wanaume wanaopenda kulelewa kwa madai ya kuwaridhisha wanawake kwenye mapenzi kwa kuwaambia kwamba hata wanawake huwa wanachoka kupigwa vizinga vya kila mara.
Nisha ametoa povu hilo kwenye FNL ya EATV na kusema wanaume wengi wanaokuwa hawapendi kufanya kazi kwa madai wanatunzwa na wanawake wanakuwa ni mzigo kwani wanawake wanaangalia mapenzi ya kweli na kama jinsi wanaume wanavyojielewa kwa kutokuwa na wanawake wanaoomba kila kitu.
“Mimi ni miongoni mwa wanawake ambao nimekuwa na mahusiano na wanaume wanaopenda kutegemea wanawake kwa kila kitu. Niweke wazi mwanaume ambaye ni tegemezi siwezi kudumu naye na huwa ninamkana kabisa mbele za watu kwamba hajawahi kuwa mwanaume wangu. Hata sisi tupo kama waaume wanaojitambua, tunasaidiana pale mtu anapokwama lakini siyo kwamba mtu ana uwezo wa kufanya kazi lakini anataka kupewa kila kitu mimi sitawezana na wewe na kama kuna mwanaume wa aina hiyo amekaa akisubiri nafasi hiyo kwangu amefeli.
Hata hivyo kwa sasa imekuwa fashion kwa wasanii wanawake wa bongo movie pamoja na wasanii wa muziki na wale waliopo kwenye urembo na mitindo kuwa na mahusiano na vijana walio na umri mdogo.
EATV.TV