-->

GK Awafungukia Wasanii Waoponda Mabadiliko Kwenye ‘Game’

Rapa mkongwe kwenye muziki wa Hip hop Tanzania ambaye kwa sasa ameachia kazi yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Mzuri pesa’ amefunguka na kusema kuwa wasanii ambao hawataki kubadidilika katika muziki au kazi zao ni kwamba hawana uwezo wa kubadilika.

gk

King Crazy GK alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV na kudai kuwa hata waasisi wa muziki wa Hip hop walibadilika hata muziki huo wa Hip hop umebadilika kwani mwanzo ulikuwa mgumu sana na sasa mambo yamebadilika hivyo si vibaya kwa msanii kubadilika na msanii anayeweza kubadilika ni yule mwenye uwezo wa kubadilika.

“Maisha yanabadilika, tunabadilika tunaangalia soko pia linataka nini, teknolojia kila siku mambo yanabadilika mwanamuziki ni kama kuogelea au kucheza mpira, muziki hauna ‘Limit’ ni limiteless unaweza kufanya chochote, mtu hawezi kumwambia sijui Misago wewe unaimba tu au una rapu tu ‘No’ yeye ni nani? Unaweza kufanya lolote ilimradi ni muziki. Watu wanakuwa wanatafsiri muziki vibaya lakini kama wewe ni mwanamuziki unaweza kufanya chochote kile” alisema GK

Mbali na hilo GK anasema Hip hop kama utamaduni toka ilipoanza mpka sasa kumekuwa na mabadiliko mengi katika utamaduni huo wa Hip hop

“Muziki ni mtazamo lakini ukitazama hata Hip hop kama ‘Culture’ toka ilipoanza kwenye waanzilishi mpka sasa imekuwa ikibadilika inakuja na sura tofauti ilikuwa ‘so hard’ watu wanavaa makufuli sijui minyororo, watu wanatukana wanawake lakini imekuja ikabadilika watu wanasifu wanawake, imebadilika watu wanaimba wana soft mwisho wa siku imekuwa muziki. Kuna watu hawataki kubadilika sababu kubadilika ni uwezo, kubadilika ni maarifa huwezi tu kusema unabadilika” alisema King Crazy Gk

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364