Naenda Kuiteka Afrika na Dunia- Baraka The Prince
Msanii wa kizazi kipya Baraka The Prince ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Siwezi’ ametangaza kuanza safari ya kulikamata soko la muziki Afrika na kisha baadaye dunia.
Baraka The Prince ambaye kwa sasa yupo chini ya Rock Star anatarajia kuachia kazi yake ya kwanza siku ya Jumanne ya tarehe 13 ambayo ni kazi ya kushirikiana na msanii Alikiba ambaye pia yupo chini ya Rock Star.
” ‘It’s almost a year tangu nilipoachia kazi yangu ya mwisho, Siwezi. Katika kipindi hiki nimepitia mambo mengi sana. Nimekuwa kiakili, kifikra na kisanaa na sasa nipo tayari kuianza safari mpya.Kufika hapa leo haikuwa kazi rahisi, pamoja na kipaji changu nilichojaaliwa na Muumba, lakini labda bila usaidizi mkubwa niliopata kutoka kwa baadhi ya watu, pengine nisingekuwa hapa leo” alisema Baraka The Prince
Mbali na kuwashukuru baadhi ya watu ambao walikuwa wakimsaidia kwenye kazi yake hiyo ya muziki mpka alipofika hapo Baraka The Prince alisema ameanza safari mpya kabisa katika muziki wake kwa kuanza kulisaka soko la Afrika na dunia.
“Leo hii September 10, 2016, natangaza kuianza safari mpya kimuziki kwenda kuiteka Africa na dunia, naomba mnisupport kijana wenu” aliandika Baraka The Prince