-->

Harmonize Afukungia Kuhusu Kuchunwa Pesa na Wolper

Mwanamuziki wa Bongo Flava anayesimamiwa na Wasafi, Harmonize, amekanusha kuchunwa pesa na mpenzi wake Jackline Wolper kutokana na mwanamke huyo kuonekana kuwa na maisha ya kifahari.

HARMONISE23

Harmonize amekanusha hayo mbele ya camera ya eNewz kwa kusema “Nyumbani kwa Wolper kuna kaunta ambayo anaweza kunywa vinywaji atakavyo, pia sioni sababu ya mimi kupendeza na mwanamke wangu asipendeleze ni lazima nitahakikisha anapendeza kwa kuwa ninampenda”

Harmonize pia alizidi kuweka wazi kuwa mapenzi yake na Wolper hayaathiri kitu chochote kwenye kusaidia familia ya kwao kwa kuwa hata kama asingekuwa na Wolper ni lazima angekuwa kwenye mahusiano.

“Siyo kwamba ninatumia pesa nyingi kumridhisha mpenzi wangu na kusahau familia yatu, Mama yangu na ndugu zangu wanapata pesa za matumizi kama kawaida kwa kuwa ninafanya kazi”

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364