Kajala Afunguka Sababu ya Kwenda Gym
Msanii wa filamu na Mama wa mtoto mmoja, Kajala Masanja amesema haendi gym ili kutafuta ‘shape’ ya mwili wake kama baadhi ya watu wanavyodhani.
Mwigizaji huyo ambaye ameachia filamu mpya ‘Sikitu’ hivi karibuni, amesema anaingia gym kufanya mazoezi ili kukabiliana na tatizo la moyo.
“Hapana shape tayari ninayo alinipa Mungu, labda naiongezea kidogo tu, nafanya mazoezi kuuweka mwili wangu fiti,” Kajala alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza, “Nilishauriwa na daktari kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na moyo, hivyo daktari aliniambia hata kama ninaendelea na dawa, mazoezi yatanisaidia zaidi,”
Pia mwigizaji huyo amewakata mashabiki wake wa filamu kuendelea kuzisupport kazi zake za filamu pamoja na filamu yake mpya ‘Sikitu’ iliyoingia sokoni mwezi uliyopita.
Bongo5