-->

Harmonize: Video ya ‘Matatizo’ ni Maisha Yangu

Msanii Harmonize kutoka katika label ya WCB Wasafi amefunguka na kusema video ya wimbo wake mpya ‘Matatizo’ inazungumzia maisha yake wakati anaitwa Rajabu kabla ya kutambulika kama Harmonize.

HAMONISE
Harmonize alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV na kudai kuna baadhi ya watu wanashangaa kuona alikuwa anaishi maisha hayo na kusema kuwa wao hawakuwahi kuona kama alikuwa akitaabika hivyo.

‘Unajua nilikuwa nataabika sema ilipokuwa natakiwa kukutana labda na wasanii, watangazaji au kwenda kwenye kituo cha Radio au Televisheni nilikuwa na feki maisha ili nionekane na mimi ni msanii mwenye malengo, ndiyo maana hata kazi zangu nilikuwa nikileta nimezitengeneza katika ubora wa hali ya juu kama kuweka cover zenye ubora kwenye CD zangu, lakini kiukweli nilikuwa naisha maisha ya shida ya kupambana sana” alisema Harmonize

Mbali na hilo Harmonize ameeleza sababu kubwa ya wimbo huo kutengenezwa na mwongozaji kutoka nyumbani si kama pesa wameishiwa kutengeneza video hiyo nje bali walikuwa wakitafuta uhalisia ya maisha aliyokuwa akiishi ambapo anaamini ingekuwa Afrika Kusini wasingeweza kuupata uhalisia huo.

“No si kama tumeishiwa pesa bali tulikuwa tunatafuta uhalisia wa kazi, maana nimeimba matatizo niliyokuwa nakutana nayo hivyo kwa hap hapa nyumbani inakuwa rahisi zaidi, kama unavyoona lile gheto ndipo nilipokuwa nimepanga hivyo ilikuwa rahisi kumpigia simu mama mwenye nyumba na kwenda kufanya, sasa unadhani uhalisia huo tungeupata Afrika Kusini? Alihoji Harmonize.

eatv.tv

Itazame ViDeo Ya Matatizo ya HarmoNize Bofya hapa –>>:Matatizo

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364