Mike: Naitamani Sana Salamu ya Thea
MSANII wa muda mrefu kwenye tasnia ya filamu Bongo, Mike Sangu amefunguka kuwa anatamani sana hata kusalimiana na mtalaka wake Salome Urassa ‘Thea’ kwani ameshakubaliana na matokeo hivyo kiu yake ipo kwenye salamu tu.
Akizungumza na gazeti hili, Mike alisema tangu watengane na mkewe huyo, takriban miaka mitatu iliyopitana hawajawahi kusalimiana kitu ambacho anaona si kizuri.
“Naitamani sana salamu ya Thea kwa kuwa salamu si jambo baya na kama mapenzi yaliisha kitambo, kujuliana hali ni kitu kizuri kwani tutanuniana mpaka lini?” alisema Mike.
Gazeti hili lilitamfuta Thea na kumuambia kuhusu suala hilo la salamu ambapo alisema:
“Sasa nimsalimie ili iweje? Kwa kweli siwezi na sina sababu ya kufanya hivyo kamwe,” alisema Thea.
Chanzo:GPL