-->

Nitakuwa Sauti ya Wengine- Wankota

KILA mwandishi wa Script anajua ugumu wake na kufanya waandishi wake wawe wachache zaidi katika tasnia ya filamu Swahilihood, mwanadada mwenye kipaji cha ajabu Wankota Kapunda kwa kupitia kipaji chake anasema kuwa atakuwa sauti ya wale wote waliopatwa na tatizo kama lake.

Wankota akiwa mwenye furaha baada ya kupiga story na wadau.

Wankota akiwa mwenye furaha baada ya kupiga story na wadau.

Wankota anawaambia FC kuwa kupitia kipaji chake anatakuwa kuwa daraja la wale wote waliopo katika matatizo ya kupooza na jamii imewaacha wakiwa pekee yao bila kuwaunga mkono katika juhudi zao za kujumuika na jamii katika ujenzi wa Taifa sehemu mbalimbali.

“Napigania nafasi yangu bila kukata tamaa nikiwaasa vijana kukimbilia ndoto zao bila kuchoka pia niwe daraja la wale waliopo katika matatizo ya kupooza na walikuwa na malengo yao kabla ya kupata ajali naamini nitawarusha katika kazi zao,”anasema Wankota.

Mwandishi huyu wa script anaamini kuwa baada ya kupatwa na matatizo kama hayo wengi wao wanajikuta wakipoteza kazi zao kama walikuwa waajiriwa, wanafunzi na kazi nyingine bila kujua kuwa wana nafasi katika jamii ni suala la kuaminiwa tu na jamii.

“Naweza kusema kuwa mimi ni mtu mwenye bahati kwani nimekuwa nisupport sana na watu mbalimbali wananipigia simu na kunipa faraja lakini najua kuna wengi wapo kama mimi na wamesahaurika hawana msaada,”

Wankota yupo Zanzibar kushiriki katika warsha ya uandishi wa Muswada (Script) iliyoandaliwa na Maisha Film Lab baada ya kuibuka mshindi kati ya washindi wa script 15 baada ya script yake kuibuka mshindi tarehe 5.Julai.2016 alitua Dar akitokea Rukwa.

Pia Wankota ametoa shukrani kwa watanzania wote ambao wamejitoa kwa ajili yake kufanikisha safari yake na bado wamekuwa watu wa karibu kwake kama Joyce Kiria, Mama Joyce Fissoo katibu wa Bodi ya Filamu, Clouds Media, Fastjet, Serena Hotel, ZIFF, Aika Gasper.

Wengine ni Kheri Mkamba mwenyekiti wa kamati ya Wankota, katibu wa TAFF Bicco Mathew, Irene Sanga, Myovela Mfwaisa, Zagamba Junior, Serikali na Watanzania wote kwa ujumla wake kwa kumuunga mkono katika harakati zake.

Filamu central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364