-->

Harmorapa Hajapokea Pesa Yoyote Katika Dili la Kinywaji cha Swala

Msanii wa Bongo Flava, Harmorapa amedai kuwa hajapokea pesa yoyote katika dili la kinywaji cha Swala tokea alipotangazwa Machi 26 mwaka 2017 kuwa balozi wa kinywaji hicho.

Akiongea na Bongo5, mkali huyo ameeleza kuwa hata yeye amesikia tetesi tu kuwa alilipwa milioni 100 licha ya kuwa hajapokea pesa hizo.

“Kwanza nizungumzia Kenya au sio, kwanza mimi nje ya muziki ni na biashara zangu na nilienda Kenya kwa issue za Business  zangu na nilivyofika kule na unajua mimi ni mtu maarufu sana nikitua tu kokote nafahamika, wakajitokeza wadau  wakasema kwanini tusifanye kitu flani hivi na maanisha show,” ameeleza msanii huyo.

Kuhusu dili la kinywa cha Swala msanii huo akafunguka “Kiujumla niseme tu kwamba baadae mimi nikaona sielewi elewi inakuaje kuwaje maana kulikuwa na maneno mengi mengi vitu vikawa haviendi  nikajiuliza kuna nini na nikaona tu niyamaze ni kaushe maana sijui chochote kinachoendelea.”

Akasisitiza “ Nilikuwa tu naona maneno maneno mtandaoni kuwa Harmorapa amesainiwa kwa dili la milioni 100 sijui nini , nikashangaa kuona mbona mimi sina hata kiasi hicho ambacho kinatajwa tajwa mitandaoni mwisho wa siku nikaona bora tu nikaushe.”

Kuhusu ukaribu  wake na mtayarishaji wa muziki nchini P-Funk, Harmo ameeleza kuwa yeye na Producer huyo hawana ukaribu kama mwanzo ila anamshukuru sana kwa mchango wake.

chanzo: udakuspecially

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364