-->

Hawaitakii Mema Ndoa Yangu – Shamsa Ford

Mwigizaji Shamsa Ford amefunguka na kusema kuna watu wengi wamekuwa si watu wema katika ndoa yake, na wamekuwa wakihangaika kuona ndoa yake hiyo inapotea au hata kuvunjika kabisa.

Msanii Shamsa Ford akiwa na mume wake Chid Mapenzi

Shamsa Ford amesema kutokana na vitendo mbalimbali ambavyo amekuwa akivishuhudia ni wazi kuwa watu wanampiga vita na kutaka kuisambaratisha ndoa yake hiyo, jambo ambalo anasema Mungu hawezi kuliruhusu kutokea.

“Nikiwa kama binadamu ni vibaya kuishi na kinyongo kwasababu natembea na umauti na sijui ni lini Mungu atanichukua. Kiukweli mmenisononesha sana binadamu, ila kubwa kuliko vyote nimegundua kwamba watu wengi hawaitakii ndoa yangu mema. Nilipoanza uhusiano na mume wangu wakasema tutachezeana na kuachana. Tulipooana wakasema hatutofikisha mwezi tutaachana, mitihani mingi iliyotutokea binadamu hawahawa walikuwa wanacheka” alisema Shamsa Ford

Shamsa alizidi kusisitiza kuwa yeye amempenda mume wake na hata aweje ataendelea kumpenda sababu ni wake yeye na yeye ndiye aliyemchagua.

“Leo hii mnatusimanga na hayo mambo mnayoposti..Nyie binadamu mnataka nini jamani..Ni wa kwangu mimi hata aweje ni wa kwangu mimi. Mnalotaka litutokee Inshaallah kwa kudra za Mwenyezi Mungu halitatokea. Pale mnapowaza mabaya yatutokee kwenye maisha yetu na Mungu naye anapanga kutuepusha na hayo mabalaa” alisisitiza Shamsa Ford

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364