-->

Haya Ndio Majibu ya Mrithi wa Kanumba Kuhusu Lulu

KUTOKANA na hivi karibuni mama wa aliyekuwa staa mkubwa wa filamu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumwanika kijana ambaye ni mwigizaji wa tamthilia, Fredy Swai kuwa ndiye mrithi wa mwanaye, kijana huyo alibadilika muonekano usoni baada ya Global TV Online kumhoji kuhusu ukaribu wake na Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyekuwa mpenzi wa Kanumba.

Fredy aliulizwa kama ana mawasiliano na Lulu, alipatwa kigugumizi na kosa jibu la moja kwa moja na alijibu tofuti na swali lilivyomtaka kujibu, katika hali ya kujilazimisha alijibu kuwa hana namba ya Lulu huku akionesha hali ya kukosa amani.

Bado haijafahamika kwa nini alisita kiasi cha kushindwa kujibu ndiyo ndio ua hapana na badala yake akakausha kwanza, baadaye akatoa maelezo.

Akizungumza na Global Tv Online, Fredy alisema hana namba ya Lulu na hajawahi kukutana na Lulu na endapo atakutana nae ataongelea kazi tu kwani amekuwa akizifuatilia sana kazi zake na si vinginevyo.

Saalum Milongo/GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364