-->

Nimeamua Kuwa Nuru Yao- Da Zitta

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu Bongo Zitta Matembo ‘Da Zitta’ aamegeukia walemavu baada ya kutengeneza filamu ijulikanayo kama Nuru huku mhusika mkuu wa filamu hiyo akiwa mlemavu kabisa na inaelezea changamoto wanazokutana nazo jamii hasa wale wenye ulemavu wa viungo mbalimbali Da Zitta anasema kuwa imekuwa ni vigumu sana wasanii ambao wana ulemavu kupiwa nafasi hata kama wana uwezo mkubwa wa kuigiza au fani nyingine ile.

Da-Zitta-2

“Nilivutwa sana na kipaji cha mtoto wa familia yetu nikaona bora niwe Nuru yao kwa sababu unakuta msanii ana kipaji lakini ni mlemavu inafikia wakati ambao mtu mzima anaigiza kama mlemavu wakati wenyewe wapo nikasema hapana ni nafasi yao sasa na ameigiza kwa kiwango cha juu sana,”alisema

Msanii mhusika katika filamu ya Nuru anaitwa Mwajuma Abdul katika filamu hiyo anaitwa Nuru na ameigiza akishirikiana na waigizaji wengine ambao si wenye ulemavu ni sinema ambayo itazinduliwa sikuya walemavu mwezi wa 12 ikiambatana na wimbo maalum ambao ni kwa ajili ya filamu hiyo ambayo itawatia moyo wale wote waliokata tamaa kwa ajili ya kuwa walemavu.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364