Hii Ndiyo Kauli ya Mwisho ya Sitta Baada ya Kuambiwa Hawezi Kupona
Mtoto wa marehemu Samweli Sitta,ambaye pia ni Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta amesema kabla ya kifo cha mzee sita alisema “that is life (hayo ndiyo maisha) baada ya kuambiwa na daktari kwamba ugonjwa unaomsumbua hawezi kupona.
Benjamini amezungumza hayo alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kutaka kujua kilichopelekea kifo cha baba yake kutokea alieleza kuwa baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume.
“Ni mzee ambaye tunampenda sana ni mzee ambaye ni baba sio tu kwa familia ya Mzee Sitta lakini ni baba kwa watu wengi, kwa masikitiko makubwa tumempoteza baba yetu kipenzi ambaye alisumbuliwa na Saratani ya tezi dume ambayo ilipozidi ilianza kushambulia viungo vingine na mguu akawa anapata shida kutembea,lakini yote mipango ya Mungu alitutoka mida hiyo ya saa saba na nusu Ujerumani ikiwa ni saa tisa na nusu alfajiri,”alisema Benjamin.
“Sasa mipango mingine inapangwa na Bunge pamoja na serikali wao ndiyo wahusika sasa hivi kwasababu ni kiongozi kitaifa lakini zaidi ya hapo naamini ndani ya hizo siku mbili tatu mwili utakuwa umekuja na watu watapata fursa ya kumuaga lakini kutakuwa na kwenda kumzika Urambo ambako naamini ndio nchi yake yeye kule ndiko aliko anzia na anakwenda kumalizia kule kwahiyo tuko kwenye majonzi nadhani taarifa na ratiba serikali Ikulu watatoa na maelekezo zaidi,”ameongeza.
Bongo5