-->

Hii Ndiyo Safari ya Muziki ya Ray Vanny

Msanii Raymond alimaarufu kama Ray Vanny amefunguka na kuweka wazi safari yake ya muziki toka ameanza mpaka kufikia hatua kuingia chini ya usimamizi wa label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz.

Raymond

Ray Vanny kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa ngaz’ kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana anasema mwanzo kabisaa alianza kuandika, akaja kurap kisha akaingia kwenye kuimba.

“Mimi nilianza kwanza kuandika, kurap kisha nikaja kuimba, kwa sababu kuimba kama kuimba, kujua vizuri kupanga sauti nimejifunza kanisani, baada ya hapo ndipo nilianza kuandika ngoma za kuimba, tulikuwa watu kama sita na wote tulienda kanisani na walituambia kuna masuala ya kwaya, kwa hiyo siku hiyo hiyo tumeingia kanisani tukaingia kwenye kwaya ya kanisa. Alisema Ray Vanny

Ray Vanny anasema akiwa kanisani ndipo alipojengeka kimuziki na kudai baadaye alikuja kushiriki katika mashindano ya Free Style wakati bado yupo shule, pia anadai kipindi ana rap kwenye mashindano kuna mtu alimwambia yeye ni mzuri zaidi kwenye kuimba kuliko kuchana.

“Niliposhiriki mashindano ya Free style  kuna mtu alinisikia nikiimba, akasema wewe upo vizuri zaidi kwenye kuimba. Basi niliendelea kurap nikashinda ki mkoa, baadaye tukashindanishwa Tanzania nzima nikashinda nikawa namba moja, kiukweli sikujua kama muziki una pesa hivi ila baada ya kushinda mashindano ya free style Tanzania nzima nikapewa mtonyo hapo ndipo niliposema haiwezekani ngoja nibadilishe filamu” alisema Ray Vanny

Hapo ndipo Ray Vanny anasema safari yake kwenye muziki ilipokolea kwani pesa zile zilimfanya kuanza kuandika ngoma zake mwenyewe, zikamfanya aanze kuimba imba hadi alipoingia chini ya usimamizi wa Tip top Connection na baadaye kuingia WCB Wasafi.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364