-->

Hiki Ndicho Chanzo cha Bifu la Vera na Huddah

Mrembo kutokea pande za Mombasa nchini kenya, Vera Sidika ametoa sababu ya kuwa na bifu na mlimbwende mwenzake wa nchini humo, Huddah Monroe, bifu ambalo limeteka vyombo vya habari kwa muda mrefu

vera na huddah

Akifunguka kwenye FNL ya East Africa Tv na Radio, Vera Sidika amesema wakati yeye akiwa Mombasa, Huddah Monroe tayari alishakuwa maarufu jijini Nairobi, lakini alipoenda ingawa walianza kwa kuwa marafiki, lakini baadaye Huddah alionyesha kutopenda uwepo wa Vera jijini Nairobi, kwani alihisi anamchukulia nafasi yake kwenye kazi.

“Bifu ambayo yeye anayo ilikuwa yeye amekuwa Nairobi na tayari alishakuwa star, na mimi nikatoka Mombasa nikaja Nairobi, ikawa kama nimeingilia career yake, ikawa anaaza bifu leo, anaanza kesho sasa inachosha, sasa mi nasemaga mambo kama hayo sitaki lakini anayaleta tu”, alisema Vera Sidika.

Vera aliendelea kusema kuwa kitendo hicho yeye hakipendi, hasa pale inapofikia hatua ya kuchafuana kwenye mitandao kwa kutoleana habari za uongo, akitolea mfano wa hivi karibuni wa Hudda kumtangaza kuwa yeye ni muathirika wa Ukimwi.

eatv,tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364