-->

Hivi Ndivyo Diamond Alivyomsaidia Chid Benz

Meneja wa wanamuziki wa bongo fleva Babu Tale ameweka wazi kitu ambacho watu wengi walikuwa hawakijui kuhusu Diamond na Chid Benz.

Chidi-Benz na diamond

Akiongea kwenye kipindi cha eNews kinachorushwa na East Africa Television, Babu Tale ameweka wazi kuwa Diamond Platnums ambaye anamsimamia, alishawahi kumsaidia Chidi Benzi kuacha madawa, kwa kwenda kumtoa damu na kumuwekea damu safi, lakini jambo hilo lilikuwa la siri ndio maana aliweza kurudia.

“Diamond alimshamtoa Chidi damu, kutoa ile yenye madawa, lakini alirudia unajua Chid anaacha na kurudia, sasa labda ndio maana ilikuwa rahisi kwa yeye kurudi kwa sababu ilikuwa siri, Damond siku hiyo alishinda hospitali kutwa nzima, akimtoa Chidi damu”, alisema babu tale.

Kwa sasa Chid Benzi amepelekwa Rehab bagamoyo baada ya kurudia matumizi ya madawa ya kulevya, na kumuathiri kwa kiasi kikubwa, na ameahidi kuacha matumizi ya madawa hayo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364