-->

Huddah: Natamani Kuwa Mke wa Rais

MWANAMITINDO maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe, amesema anatamani siku moja aje kuwa mke wa rais ili aweze kuishi kwa amani katika maisha yake.

Mrembo huyo wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya, alitumia mitandao yake ya kijamii kuonesha wazi kumpigia debe Rais Uhuru Kenyata.

Hata hivyo, baada ya Uhuru kushinda urais, Huddah alisema anatamani kwenda kuishi mji wa Gatundu anakotokea rais huyo.

“Kila mtu ana maamuzi yake, wapo ambao wanataka kwenda kuishi Canaan, lakini kwa upande wangu natamani kwenye kuishi anakotokea rais Uhuru, najua nikiwa huku watu wataanza kusema mengi kwamba nimekuwa mke wa pili wa rais, hata hivyo natamani kuja kuwa mke wa rais,” alisema Huddah.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364