Kisa cha Koletha Kumwacha Mwanaye
STAA wa filamu aliyeshinda shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoendeshwa na Kampuni ya Star Times, Koletha Raymond atamuacha mwanaye aliyejifungua hivi karibuni mwenye umri wa miezi nane kufuatia kupata kazi nchini China.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Koletha ambaye alishika namba moja kwenye shindano hilo alisema baada ya kushinda pamoja na wengine wana mkataba wa mwaka mmoja wa kwenda kufanya kazi jijini Beijing.
“Mume wangu amenipa ruhusa maana ni mwanaume mwelewa na anayenisaidia kwa kila nifanyacho, tunashikamana katika shughuli zetu hivyo ameridhia mimi kuondoka na mtoto nimwache kwa mama yangu, nimefurahi sana kwa ushindi huu kwa kweli maana umenipa fursa ambayo sikuitegemea,” alisema Koletha.
Chanzo:GPL