-->

Huu Mwaka Una Mambo Mazuri Utakuwa Mwaka wa Kumbukumbu

February 5, 2018 Staa wa Bongofleva na President wa WCB Diamond Platnumz azidi kuwaahidi mashabiki zake vitu vikubwa kuhusu muziki wa Bongo Fleva kufanya vizuri zaidi kwa mwaka huu wa 2018 ameyasema haya kupitia account yake ya instagram.

Ambapo mwanzoni wa mwaka huu wa 2018 ameanza kwa kumtambulisha rasmi Mbosso WCB pamoja na kazi yake mpya ambapo mashabiki wameupokea vizuri wimbo huo

Kupitia instagram yake ameaandika caption inayosema “Matangazo ya siku 4 Mitandaoni na #WATAKUBALI ikiwa inasiku sita tu tangu itoke, Dah!….sio kwasababu eti tunaakili na kujua sana Hapana! ni kwasababu Mnatupenda na kutusapoti sana…Baraka za Mwenyezi Mungu, lakini pia Mnaridhika na kuvipokea vidogo vyetu tunavyowapatia.”

“Kwakweli Tunawashukuru na tunawapenda sana huu mwaka una mengi sana mazuri juu ya hii sanaa mengi sana naamini utakuwa ni mwaka wa kumbukumbu kwenye hii nchi ni mwaka ambao utaleta nyuso ya furaha kwa Wasanii, Mashabiki, na wadau wote wa sanaa tuseme InshaAllah”

Ukiachilia mbali na utambulisho alioufanya kwa Mbosso, Diamond Platnumz ametuonyesha jengo la Headquaters mpya za WCB ambapo pia zitapatikana ofisi za Wasafi Tv na Wasafi FM ikiwa ni moja ya kumbukumbu za mwaka huu wa 2018.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364