-->

Fid Q Amuweka Wazi Mpenzi Wake Awapiga Stop Wanawake Wanaomsumbua

Fid Q Amuweka Wazi Mpenzi Wake Awapiga Stop Wanawake Wanaomsumbua

Mkali wa HipHop Bongo Fid Q ameonekana kukamatika kimahaba kwa  mrembo ambaye amemtambulisha nyumbani kwao Mwanza na ameiambia eNEWZ kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano rasmi.

Fid Q amesema ameamua kupost picha kwenye mitandao yake  ya kijamii ili kupunguza wasichana wengine kumtumia meseji za kumsumbua lakini pia kuwaonyesha mashabiki zake kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi kwani umri wake unaruhusu.

”Nimeamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kuzuia usumbufu wa kina dada wanaonisumbua katika mitandao ya kijamii na hata ninapokuwa kwenye viwanja vya starehe na mda wowote kuanzia sasa ninaweza kutangaza ndoa”, amefunguka.

Kwa upande wake mrembo huyo wa Fid amesema hawashangai sana wanawake wanaomtongoza Fid kwenye ‘Social network’ kwa kuwa mpenzi wake anamuonekano mzuri na ni mwanaume ambaye ameshapitia mambo mengi duniani hivyo anaamini kwamba atakuwa mwanaume bora kwake.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364