-->

Huyu Ndiye Gabo Zigamba Mjukuu wa Mzee Kiyeyeu wa Iringa

Gabo-zigamba-21

Gabo Zigamba mwigizaji wa filamu

UNAPOSIKIA jina la Gabo Zigamba si jina geni katika tasnia ya filamu , Gabo amejizolea umaarufu katika tasnia ya filamu baada ya kufanya vizuri na kuwachanganya wapenzi wa filamu Bongo, wengi wakiamini kuwa ni kijana wa Kimachinga kutoka Kusini kumbe ni Mdigo na Mhehe.

Jina halisi la msanii huyu ni Salim Ahmed Issa akisema hilo ni jina la kliniki, lakini jina la riziki anajulikana kama Gabo Zigamba, amezaliwa Mitaa ya Mshindo na kukulia katika mitaa ya Kitanzini kama ingekuwa hapa Dar ni mtoto aliyezaliwa Ilala na kukulia mitaa ya Kariakoo akilelewa na mama yake Rafia Issa Kiyeyeu.

Babu yake ni Mtogapaafwe Kiyeyeu familia ya Martin Kiyeyeu mtu maarufu sana Iringa ambaye kila unapotaja jina lake wengi ukumbuka kuhusu maajabu ya kaburi lake, Gabo anasema kuwa ameishii pande zote mbili lakini sehemu kubwa sana ni Iringa kwa mama yake akisoma Ipogolo Iringa.

Gabo anasema yeye ni mwanaharakati sauti ya wanyonge isiyosikika hivyo alianza harakati zake kitambo akifiria ni jinsi

 

anavyoweza kufikisha ujumbe kwa jamii husika kwa kupitia sanaa na hasa filamu, wengi wanaamini kuwa sinema yake ya kwanza ni Bado Natafuta lakini ni kazi ilifanya vizuri baada ya kupewa nafasi.

SANAA ALIANZA LINI
Gabo kuigiza alianza kitambo lakini rasmi ilikuwa ni 2006 kwa kushiriki katika vikundi mbalimbali huku akiwa na shauku kubwa ya kuwa nyota na kufikia lengo lake la kuwatetea wasio na nafasi anasema haikuwa rahisi sana kwani kulikuwa na changamoto nyingi ambazo hazikumkatisha tamaa.

Harakati zangu hazikuja kama upepo sinema yangu ya kwanza ilikuwa ni Olopong iliyotengenezwa na Al Riyamy Production chini ya Khalfan Abdalah, hapo milango ndio ilifunguka kwani baada ya hapo nikacheza 007 Boyz,”anasema Gabo.

Baada hapo alishiriki katika filamu ya The Plan, na kujiunga na kampuni ya marehemu Juma Kilowoka ‘Sajuki’ Wajey Film akishiriki katika sinema zao kama mwigizaji na kufanikiwa kucheza filamu Mchanga na Keni, The killer na 007 Days alikuwepo hapo akijifunza vitu katika tasnia ya filamu.

Gabo-23

Gabo akiwa na Irene Uwoya, Chopa, Chuchu Hans, Richie katika filamu ya Safari.

Filamu nyingine alizoshiriki ni Majanga, Safari, Fikra zangu ya Jerusalem Film ya Jb hizi zote zikiwa za watayarishaji wengine tofauti na filamu yake ya Kona ambayo aliitayarisha mwenyewe, na sasa amekuja na filamu yake ya Safari ya Gwalu inayoelimisha jamii ikiwa imetayarishwa na yeye.

Mtayarishaji Vipindi na Mtangazaji
Gabo ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Bondeni kipindi kinachorushwa katika televisheni ya Taifa ya TBC1 ambacho kinafuatilia maisha ya ughaibuni, na kimekuwa kivutio sana kwa watazamaji wakishuhudia maisha magumu ya ugenini hasa wale walioenda bila mipango thabiti.

“Kama nilivyosema awali kuwa mimi ni sauti ya wanyonge wasiosikika nikaona filamu tu haitoshi kupaisha sauti za wanyonge chini ya menejimenti yangu tukaja na kipindi cha Bondeni,”

Gabo ameshatengeneza vipindi vingi sana katika nchi za Afrika ya Kusini, Zambia, Botswana, Uganda na Malawi na hivi karibuni anatarajia kwenda nchini Oman kwani kuna watanzania wengi ambao wanapata shida kwa sababu ya uvivu wa kutofanya kazi.

“Safari zangu za kurekodi kipindi cha Bondeni imekuwa ikipata ushirikiano na balozi za Tanzania kwani wao ndio wanatuelekeza sehemu wanazopatikana watanzania, kwa mfano Oman tumeambiwa watanzania wamekwama na sababu kubwa hawataki kufanya kazi,”

“Baadhi ya watanzania wamekuwa wakikimbilia maisha ya ughaibuni huku ni wavivu wa kujishughulisha, Balozi mmoja ametueleza sisi tunaweza hata kumtukana bosi kwa sababu ya uvivu wetu,”

Tuzo
Ili huweze kuonyesha ubora wako na umahiri katika fani yoyote ni pale unapokumbukwa na taasisi au chombo chochote kwa kutambua mchango wako katika kile unachofanya, Gabo ana tuzo mbili moja ni Mwigizaji wa bora wa kiume kupitia tuzo za Action & Cut Views Choice Awards 2014/2015.

Pia mwaka huu aliweza kujishindia tuzo nyingine kutoka nchini Kenya kwa kupitia sinema aliyoshiriki ya Queen Masai akiwa kama mwigizaji bora tena wa kiume.

Changamoto
Gabo anasema kuwa amekutana na changamoto nyingi lakini yeye kwake ilikuwa ni chachu ya mafanikio kwani kwani baada ya kushiriki filamu za watayarishaji wengine aliamua kusambaza kazi zake mlango kwa mlango kupitia Sarafu Media kutokana na mizengwe ya wasambazaji.

“Sitaki kujiita jeshi la mtu mmoja kwa ni alama ya mtu kajiita mimi ni hazina yenye madini joto, wakati tunaanaza kusambaza filamu ya Safari ya Gwalu vikwazo vilikuwa vingi hadi nikaamua kuzunguka na timu yangu kila wilaya,” anasema Gabo.

Changamoto nyingine ni wakati wakati wa kutengeneza vipindi kusafiri kwa muda mfupi na kufanya kitu ambacho kinakuwa bora lakini kuna wakati watakutana na watanzania wamechoka wanahitaji msaada wa kurudi Bongo tu lakini hawana nauli wakihitaji msaada kwake.

gabo-4

Gabo akipokea tuzo kama mwigizaji Bora 2013/2014

Faida
Gabo anasema moja ya faida kubwa kwake ni pamoja na kupata marafiki wengi kutoka sehemu mbalimbali lakini faida kubwa kabisa ni kuwa balozi maji ambayo yatazinduliwa hivi karibuni kiwanda ambacho kitajengwa na Mtanzania anayeishi Malawi Bishop Simama mfanyabiashara mkubwa sana nchini Malawi.

Katika kuenzi ukoo wa mama yake yaani akina Kiyeyeu Gabo amepanga kutengeneza filamu kubwa ya kufungia mwaka huu itakayojulikana kama Nyumba niitu sehemu maarufu kwa kuabudia Wahehe kama zawadi kwa babu zake akina Kiyeyeu na kuimarisha mila na Tamaduni za Babu zake.
Huyu ni Gabo Zigamba maarufu kama Chinga huku akisema yeye ni Chotara wa Kihehe na Kidogo tena wale wadigo wa Mombasa Kisauni.

Chanzo: Filamucentral

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364