Idris Athibitisha Kumpa Wema Ujauzito
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2015 Idris Sulta, athibitisha kumpa ujauzito mlimbwende amabaye hakauki vinywani mwa watu kutokana na umaarufu wake na urembo wake Wema Sepetu, huku akijivunia kuwa na mwanamke huyo maishani mwake.
Katika ukurasa wake wa Instagram Idris Sultan ameandika maneno ambayo yanaashiria wazi mlimbwende huyo ambaye pia anafanya vizuri runingani kwa filamu za kibongo, kuwa ni mjamzito na yeye akiwa ndiye baba wa mtoto huyo, huku akisindikiza na ujumbe wa mahaba kwa mwenzi wake huo.
“Me and You are not the ordinary. I sleep, eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama “Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike” aliandika Idris kwenye ukurasa wake.
Idris aliendelea kwa kumwagia sifa mrembo huyo ambaye amekuwa gumzobaada ya kuwepo kwa tetesi za kunasa ujauzito huo.
“I might bring you the most beautiful rose flower in the world and it will never look even half as beautiful as you are. When you’re jealous unasonya sonya, when am jealous i smile. I would move mountains and planets just to make you happy. I will protect you, love you, spoil you, fight with you, cook with you, watch movies together, drive at night for no reason, sit with you and just stare at the stars, you’re more than i ever asked for, you’re my everything, my wife”, aliandika Idris.
Kwa upande wa Mashabiki wameonyesha kufurahishwa na kitendo hicho na kuandika yale yaliyomo kwenye hisia zao.
Sheylerf : Idris nakuombeeni khery umuoe wema awe mkeo mfanye yote kihalali wallah nawapenda sana Allah awabarik awajaalie muonane muish kihalali what a great dady Masha Allah Wema Sepetu japo hujui ila huwa nakuombea sana upate mtoto Allah akuhifadhi akuepushe na hasad, fitna na balaa zote akujaalie kizaz chema uzae mpka ushangae u deserve being happy Idris plz fanya vile uislam unaelekeza oaneni na muijaze dunia
Cyahminja : Uuuwi cjawahi comment ila leo am soo touched jamani those are the most sweetest words a girl cud hear from her bae.. I would die to hear smone tel mi dc.. Idris ure smthing.. Wema u re a lucky woman.!happy for u guys.. God bless you jamani khaa hadi chozii.
Wema Sepetu ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji maarufu wa filamu nchini, amekuwa akilalamika kuhusu suala lake la kutopata mtoto kwa muda mrefu, na sasa mpenzi wake huyo ameweka wazi jambo hilo ambalo wengi wamefurahia.
eatv.tv