-->

Idris Sultan Ana Utani na Jack Wolper!

IDRIS Sultan muigizaji wa filamu na mchekeshaji mahiri katika masuala ya komedi ametoa kali ya mwaka pale alipojaribu kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya akimzodoa muigizaji mwenzake katika tasnia ya filamu swahilihood Jack Wolper kwa kumwambia kuwa msanii huyo wa kike kwa mwaka huu amefunga mwaka kwa kutendwa na wanaume.

Idriss Sultan muigizaji wa filamu

“Kiukweli inatia huruma sana ninapokutana na msanii mwenzangu Jack Wolper kila anapochangua mwanaume lazima alie, kwa mwaka 2017 Wolper amekuwa na idadi kubwa ya wanaume kuliko single alizotoa Ali Kiba,”alisema Idris.

Jack Wolper

 

 

Akiongea huku akicheka msanii huyo amedai kuwa mara kadhaa Jack amekuwa akimpata mpenzi mpya anamtambulisha kwa mbwembwe lakini siku ya siku utasikia akilia kwa madai kuwa ametapeliwa na mwanaume huyo kumbe hakuwa muoaji na pengine amemchuna na kumpotezea muda wake, anamsihi awe na siri moyo wake utakuwa na amani.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364