Idris: Uhusiano Wangu na Wema ni ‘Private’
Hutoona tena Idris Sultan na Wema Sepetu wakionesha upendo hadharani kama zamani kwakuwa wameamua kuuweka ‘private’ kwa sasa.
Mshindi huyo wa BBA 2014, ameiambia Bongo5 kuwa angependa zaidi kwa sasa kujikita kwenye kazi zake kuliko kuufanya uhusiano wao uwe mjadala mkubwa.
“Sipendi uhusiano wangu uwe kitu kikubwa kuliko kazi yangu kwa sasa,” alisema.
Hata hivyo kama wasemavyo wahenga kuwa penzi ni kikohozi huwezi kukificha, Wema ameonekana kutilia mkazo jinsi ambavyo anampenda staa huyo kwa comments za hapa na pale kwenye post za Instagram.