-->

Irene Uwoya Afungukia Ndoa Yake

IKIWA hali ya sintofahamu imeendelea kutanda kuhusu ndoa ya msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja ‘Janjaroo’ na mwigizaji, Irene Uwoya, picha za shughuli yao zimezidi kusambaa.

Uwoya, ambaye alishiriki Miss Tanzania 2006, amekuwa akituma picha hizo za harusi katika mitandao ya kijamii na mumewe, Janjaroo kujibu.

Hali hiyo imekuwa gumzo mitaani huku wengi wakishindwa kupata jibu moja kama ni kweli wawili hao wameoana ama ni video ya wimbo mpya wa Janjaroo ama ni filamu mpya ya Uwoya.

Pamoja na hayo, Uwoya ambaye aliwahi kuolewa na nyota wa zamani wa Stand United, Mnyarwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, alipiga stori mbili tatu na Mwanaspoti na kujibu maswali machache tata, ambayo yamekuwa yakiwatatiza mashabiki wake.

MWANASPOTI: Mwanzoni mwa mwaka huu, ulisema kuwa hutaolewa mpaka miaka mitano ipite, imekuwaje tena kutangaza kuwa umeolewa hivi karibuni?

UWOYA: Ni mabadiliko tu yametokea kwani hayo ni maamuzi yangu. Hakuna mtu anayeweza kunichagulia kitu cha kuamua.

MWANASPOTI: Inasemekana hii ndoa umelazimishwa, japo baadhi ya watu wanadai sio ndoa ya ukweli ila kuna kitu mnahitaji kuwapa mashabiki wenu?

UWOYA: Sijalazimishwa kuolewa na Dogo Janja, ila watu ndio wanalazimisha maneno wanayoyaongea yakubalike kwa wengine tena bila ya kukubali kinachoongelewa na wahusika ambao ni sisi.

MWANASPOTI: Vipi kuhusu mume wako Ndikumana ameshakupa talaka?

UWOYA: Siko naye, jua tu niko huru kufanya chochote bila pingamizi lake.

MWANASPOTI: Ukiachana na mambo ya ndoa, kwenye maisha ya kawaida, ni vitu gani huwa vinakuudhi sana?

UWOYA: Huwa naudhika zaidi na vitu vidogo kuliko vitu vikubwa.

MWANASPOTI: Ulishawahi kumsamehe mwanaume aliyekusaliti?

UWOYA: Niko tofauti na wanawake wengine aisee, yaani sijawahi kumsamehe mwanaume aliyenisaliti na sitaweza. Mwanaume akijua tu amenisaliti na nikagundua, ajue safari imemuita.

MWANASPOTI: Huwa unashika simu ya mpenzi wako?

UWOYA: Hapana, sijawahi na sipendi kabisa kushika, napenda awe huru.

MWANASPOTI: Tuambie wewe ni mtu wa aina gani?

UWOYA: Mimi ni mpole, mcheshi na napenda watu, japo baadhi ya watu wanahisi mimi ni mkali.

MWANASPOTI: Ulishawahi kupigana au kumpiga mtu?

UWOYA: Ndio, tena sana tu, maana huwa sitaki mtu aniletee ujinga, nina hasira.

MWANASPOTI: Unapenda mwanaume wa aina gani na unavutiwa na nini?

UWOYA: Mkweli, asiwe muongo na asiwe na sifa za kijinga. Asiwe mtu wa kujisifu mbele za watu hasa kutaja vitu alivyonavyo, na awe na pesa za kawaida tu.

MWANASPOTI: Ulishawahi kugombania mwanaume?

UWOYA: Hapana! Siwezi kugombania mwanaume na haitatokea hiyo.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364