-->

Irene Uwoya Atoa Wito Huu Kwa Wasanii Wenzake

MKALI wa filamu nchini, Irene Uwoya, amewataka wasanii wenzake hasa wanawake kujituma katika kazi nyingine kama vile biashara ili kuweza kujikomboa kimaisha.

IRENE UWOYA89

Irene amesema wasanii wengi wanategemea sanaa ili kuweza kuendesha maisha yao, lakini wanatakiwa kufanya mambo mengi ili kuweza kujiingizia kipato.

Akizungumza na MTANZANIA jana alisema yeye ana ofisi ambayo inajishughulisha na ushonaji wa nguo za aina zote ambayo inamsaidia kuingiza kipato na huwa anashona.

“Natumia kauli mbiu ya hapa kazi tu kwani mtu huwezi ukategemea kitu kimoja na hasa sisi wasanii huwezi ukategemea sanaa lazima utafute kitu kingine ambacho kitaweza kukusaidia,” alisema.

Alisema ni vema mtu akajiongeza katika kazi yenye uhalali ili aweze kufanya vitu vya msingi ambavyo vitamfanya kuendesha maisha yake.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364