-->

“Sijatoka Endless Fame” – Mirror

Msanii Mirror ambaye yuko chini ya Endless Fame amekanusha taarifa za kutoka kwenye kampuni hiyo ambayo inamsimamia kwenye kazi zake, baada ya tetesi kuwa hayupo tena.

Mirror Endless

Mirror ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na EATV, na kusema kuwa bado yupo kwenye kampuni hiyo, ingawa hasimamiwi na Petit Man, ambaye alikuwa anamsimamia awali hapo Endless Fame.

“Mimi bado niko Endless Fame ila sifanyi kazi na Petii, unajua Endless Fame ni kampuni kubwa inayofanya kazi za muziki, movie na wengine, kina Petii, Kina Martin Kadinda wapo pale, ila mi nipo Endless Fame”, alisema Mirror.

Pia Mirror amekanusha taarifa kuwa wasanii wengine Nuh Mziwanda na Nedy Music ambaye hivi karibuni alimuelezea Petii Man kuwa ni kama baba kwake kutokana na msaada anaompa, kujiunga na kampuni ya Endless Fame.

“Thats not true kwa sababu ratiba ya kampuni kama kuna msanii mwengine mimi nitaambiwa, kwa sababu hata mara ya kwanza alipokuwepo msanii mwingine nilitambulishwa huyu ni msanii mwenzako, kwa hiyo hiyo haina ukweli wowote”, alisema Mirror.

Pia Mirror amekanusha taarifa za kutumia madawa ya kulevya, na kukiri kutumia pombe na kuwa na marafiki wengi wa kike.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364