-->

Ivan Kuzikwa Leo, Zari Aahidi Kuwaangalia Watoto

Baada ya Jumatatu hii mwili wa Ivan Ssemwanga kuagwa na kufanyiwa ibada takatifu, aliyekuwa mke wa zamani wa marehemu, Zari Hassan alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya kwanza.

Katika misa ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Namirembe mijini Kampala, Uganda Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae.

Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhuria walijianda kumsikiliza atakachosema.

“Sitomhuzunikia Ivan,” alisema. “Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu, tulitengana kwasababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan. Ivan alijua kile nilichoweza kufanya. Alijua kile nilichoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua kuwa ningewaangalia vijana vyema na aliniamini. Kwa hali hiyo, naahidi ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye.”

Ivan anatarajiwa kuzikwa leo ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili naye aliahidi atahudhuria.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364