-->

Ridhiwani: Baba Alinitoa Hofu

Dar es Salaam. Baada ya kuitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema taarifa hizo zilitingisha familia yake, lakini baba yake Jakaya Kikwete alimtia moyo.

Ridhiwani Kikwete

Tofauti na watuhumiwa wengine waliohojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, Ridhiwani hakutangazwa hadharani badala yake aliitwa kimyakimya na kuhojiwa na baadaye kuruhusiwa aendelee na shughuli zake baada ya kuonekana hana hatia.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ridhiwani amesema JK hakushtushwa na badala yake alimpa nguvu ya kwenda kueleza ukweli .

“Pengine aliamua kuficha hofu yake ili kunitia nguvu,” amesema Ridhiwani.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364