Jb Awashukia Wasanii Wenzake Kuhusu Hili!
JACOB Stephen ‘JB’ msanii mahiri katika tasnia ya filamu Bongo amewashukia wasanii wenzake kwa kusema kuwa wengi hawapo makini na tasnia jambo ambalo linawafanya kupoteza mapato mengi kutokana na tasnia hiyo bila sababu.
Ukweli ni kwamba wasanii wengi hawapo serious na kazi kitu kinachofanya tukose pesa kwenye filamu, na ukitaka kutambua hilo angalia page zao za Instragaram wanachoposti,”anasema JB.
JB amesema kuwa mara nyingi wasanii wamekuwa wazito sana katika shughuli zinazowahusu wao kujitokeza kushiriki jambo ambalo linafanya mambo yao yaongelewe na watu ambao si wadau wa filamu JB alisema hayo Suncrest Cinema ilipoonyeshwa sinema ya Nimekosea wapi?
Siku hiyo pamoja na tukio hilo kuwa ni wasanii lakini hakukuwa na waasanii waliojitokeza zaidi ya wapenzi wa filamu na wadau wengine kama watengenezaji na wanahabari tu katika uzinduzi wa uonyeshaji wa filamu kwenye majumba ya sinema.
Ripoti na Filamucentral
FANYA BISHARA YA KUUZA FILAMU KUTOKA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT
PIGA NAMBA HIZI: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA