-->

Malaika Akiri Kutengana na Mpenzi Wake

BAADA ya kufanya siri kwa muda mrefu, staa wa Ngoma ya Raruararua, Diana Exavery ‘Malaika’ amekiri kwa mara ya kwanza kuwa hayupo tena na mpenzi wake, Eddy ndiyo sababu hata ya kufikia hatua ya kuondoka walipokuwa wakiishi pamoja Kunduchi jijini Dar.

malaika23

Diana Exavery ‘Malaika’

Akizungumza katika mahojiano mafupi na Over Ze Weekend, Malaika ambaye awali alikuwa akisimamiwa na Eddy, kwa sasa yupo chini ya udhamini kutoka Norway alikuwa na haya ya kusema;

Over Ze Weekend: Ningependa kupata ukweli, ni kweli umeachana na mpenzi wako maana maneno yamekuwa mengi sana.
Malaika: Ni kweli hatuko pamoja tena kama zamani, kwa sasa hivi niko na mambo yangu na yeye vilevile.
Over Ze Weekend: Lakini mbona inasemekana kuwa yeye ndiye alikuwa mpango mzima katika muziki wako wote?
Malaika: Hapana! Kwa sababu niliruhusu watu waamini hivyo lakini haikuwa hivyo.

Over Ze Weekend: Hujafikiria kurudisha moyo na kurudi ili muendelee kuishi?
Malaika: Duh! Hapana kwa sasa na hata kama ningekuwa nafikiria kurudi ingekuwa ni ngumu kutokana na  alivyojitahidi kunichafulia katika kazi zangu.

Over Ze Weekend: Kwa hiyo uko tayari kwa mtu yeyote akitokea na kuanzisha uhusiano mpya?
Malaika: Hapana kwa sasa, maana nimejifunza mambo mengi sana katika mapenzi na ninahitaji muda mrefu sana  kwa sasa naangalia kazi zangu ndiyo.

Over Ze Weekend: Ila inasemakana jamaa amekutoa mbali sana.
Malaika: Hata mimi nasikitika kwa hilo kwa kuwa tumetoka mbali lakini matendo yake yamenifanya kuondoka kwake na hata kama anatangaza ana masikitiko kuachana na mimi nitashangaa kwa kuwa nina ndugu zangu hakuniokota.

Chanzo:GPL

FANYA BISHARA YA KUUZA FILAMU KUTOKA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT

PIGA NAMBA HIZI: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364