-->

Jimmy Master Aingia na Filamu ya Foundation Sokoni!

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu za mapigano Bongo Jimmy Mponda ‘Jimmy Master’ ameamua kusambaza kazi yake ya Foundation kufuatia mikataba inayobana watayarishaji na wasanii kutoka kwa wasambazaji wengine hivyo msanii huyo mkongwe na mahiri katika sinema za mapigano anasimama mwenyewe kuingia sokoni.

foundation-531

Filamu ya Foundation imengia jana sokoni na inapatikana nchini kote katika maduka ya kuuza filamu za Kitanzania, akiongea na FC Jimmy Master amesema kuwa kazi hiyo inasambazwa chini ya kampuni ya Mzimuni Theatre Arts, na imemshirikisha mkali mwingine Ispekta Seba na wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahilihood.

foundation-picha

Miamba wawili Jimmy Master na Ispt. Seba

“Kwa sasa vikwazo vingi katika usambazaji na masharti ya upande mmoja toka nilipoanza kazi ya filamu nimekuwa makini sana katika kulinda hai zangu kulikwepa hilo kazi yangu ya Foundation naisambaza mwenyewe nahitaji sapoti,”alisema Jimmy Master.

Jimmy amefanikiwa kuungana na mpinzani wake katika filamu wanapokutana Seba Mwanangulu katika kumshirikisha katika sinema ya Foundation ambayo Jimmy anasema inarudisha hadhi ya kazi yake iliyofanya vizuri ya Misukosuko, sinema hiyo itasambazwa kupitia kampuni yake ya Mzimuni Theatre Arts.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364