Jina Analotumia Baraka ni Langu – Dully Sykes
Mwanamuziki mkongwe Prince Dully Sykesy ameweka wazi yeye ndiye aliyempatia jina la kisanii Baraka The Prince miaka kadhaa iliyopita kabla hata msanii huyo hajatoa wimbo hata mmoja.
Katika ukurasa wake wa instagram Dully ameandika kwamba baraka aliwahi kumpigia simu na kumwomba amchagulie jina ambalo litamfanya awe maarufu.
“Kuna siku ila mwaka sikumbuki nilipata simu kutoka kwa kijana aliejitambulisha kwa jina la BARAKA. Akanisalimia na kunambia anahitaji nimpatie jina ili alitumie kwenye sanaa….nikamuuliza anaishi wapi?…akanambia anaishi MWANZA…nikamwambia nitampatia jina moja kati ya majina yangu…..ndipo nikampatia ‘PRINCE’ nikamwambia ajiite ….BARAKA DA PRINCE, na kweli….nashukuru mungu yamekuwa na amekuwa mmoja kati ya wasanii wanaonipenda na kuniheshimu ….. @barakahtheprince_ nakupenda sana mdogo wangu!..” Amefichua Dully Sykes
Hata hivyo Baraka amesikika akisema kuwa ni kweli aliwahi kufanya kitendo hicho na kwamba ni miaka mingi sana imepita na anashangaa kitendo cha Dully kutunza kumbukumbu za muda mrefu kiasi hicho.
“Niliwahi kusikia Dully akikupa jina lazima uwe maarufu , nilimpigiaga simu nikajitambulisha kwake nikamueleza shida yangu akanambia nimpigie baadaye, sikukata tamaa baadaye nikampigia akaniambia mimi natoka kwenye ukoo wa kifalme kwa hiyo nakupatia jina langu la ‘Prince’ hivyo utakuwa ‘Baraka Da prince’. Namuheshimu sana ni kaka anayenijali mimi na kazi yangu”. Amesema Baraka
Pamoja na hayo Baraka baada ya kusaini mkataba wa lebo ya Rockstar4000 inayosimamia kazi za wasanii Alikiba na Lady Jaydee, ilimbadilisha jina kutoka kwenye ‘Baraka Da Prince’ na kuwa ‘Baraka The Prince’.
EATV.TV