Mboto: Ningetembea na Aunt Ningefurahi
Mwigizaji wa Vichekesho Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ ameibuka na kufunguka kuwa iwapo angetembea na Aunt Ezekil angefurahi na angeweka wazi kwa sababu yeye ni rijali.
Mboto alisema hayo baada ya kuibuka maneno mtandaoni kuwa, Aunt aliwahi kuwa na ujauzito wake na akautoa, ishu ambayo Mboto aliikana vikali. Mboto aliliambia Wikienda kuwa, yeye na Aunt hawajawahi kuwa na uhusiano na endapo wangeingia kwenye uhusiano angefurahi na angetangaza wazi kwani yeye ni rijali anayejiamini.
“Hili suala ndiyo kwanza nimelisikia lakini kiukweli kungekuwa na ukweli wowote ningeanika kwani ni suala la kujivunia,” alisema Mboto
Chanzo:GPL